- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC MONGELLA ATAKA KUONDOLEWA MACHINGA KWENYE MIFEREJI
Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka wakurugenzi watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwaondoa mara moja wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika mifereji ya kupitisha maji.
Mongela amewaeleza John Wanga (Ilemela) na Kiomoni Kibamba wa Halmashauri ya Jiji leo Jumatano Oktoba 30, 2019 katika kikao cha kwanza cha bodi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mkoani Mwanza.
Amesema wafanyabiashara wadogo wametumia uhuru waliopewa na Rais John Magufuli kupitiliza na kuanza ujenzi wa vibanda katika mifereji ya maji mbele ya nyumba za watu kitu ambacho sio sahihi.
“Sasa hivi ndugu zetu wale si kwamba ni wamachinga tena, ni wafanyabiashara wakubwa unakuta mtu kajenga duka kwa kutumia grili na mabati na kuchomelea.”
“Na utakuta nyuma yake kuna duka ambalo mmiliki wake analipa ushuru, ana leseni ya biashara na analipa kodi TRA, hapa ni kama tunajipiga risasi mkononi,” amesema Mongella.