- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC MANYARA AMPA SIKU 7 MKURUNGEZI MBULU KUHAMIA DONGOBESH
Mbulu. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amempa siku saba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga, kuhamia katika Kata ya Dongobesh kwenye makao makuu mapya ya halmashauri hiyo.
Lakini kwa upande wake, Kamoga ambaye alikuwa mwanahabari amesema walishaanza mchakato wa kuhamia kwenye kata hiyo ili kusogeza huduma karibu na jamii.
Mnyeti ametoa agizo hilo jana Oktoba 28, 2019 wakati akikagua ujenzi wa majengo ya makao makuu mapya ya halmashauri ya wilaya ya Mbulu yanayojengwa kwenye Kata ya Dongobesh.
Amesema agizo la Rais John Magufuli alilolitoa la kila halmashauri ihamie kwenye eneo lake linapaswa kufanyiwa kazi kwa kutekeleza na kuhama mara moja. “Nilikuwa nakupa siku saba pekee za kuhama ila kwa sababu umesema umeanza utekelezaji basi nakutakia kila la heri muhamie Dongobesh,” amesema Mnyeti.
Pia, amewataka wananchi wa Kata ya Dongobesh kuwapa ushirikiano watumishi wa halmashauri hiyo wanaohamia kwenye eneo hilo.