- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC GAMBO ASEMA HANA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE ARUSHA
Arusha. Mkuu wa mkoa wa Arusha (RC) Mrisho Gambo amesema kuwa hana nia hata kidogo ya kutaka kugombea ubunge wa Arusha mjini kama ambavyo uvumi umekuwa ukienea kila kukicha nchini Humo.
Kauli ya RC Gambo ameitoa Jana usiku Jumatatu Septemba 30 wakati Akizungumza katika mkutano wa Jumuiya ya wanawake wa CCM (UWT) mko Arusha alisema nafasi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ambayo ameteuliwa na Rais John Magufuli inamtosha.
"Nafasi niliyonayo ni kubwa, wakuu wa wilaya wote wapo chini yangu, wabunge wote wapo chini na taasisi zote za Arusha zipo chini yangu, wabunge wamekuwa wakija kuniomba niwasaidie lakini mimi kama RC naagiza tu," alisema. Gambo alisema bado anahitaji kuunyoosha mkoa wa Arusha.
Tayari Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alikwisha kumkaribisha Gambo kwenye kinyang'anyiro cha ubunge katika uchaguzi mkuu ujao 2020 huku akimweleza ajipange vizuri.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha, Joseph Masawe alisema tangu Mkuu huyo wa mkoa afike Arusha, mji wa Arusha umetulia hakuna vurugu na watendaji wa serikali wanafanya kazi nzuri kutekeleza ilani.
Kwa muda mrefu, Gambo ambaye amekuwa na makazi ya kudumu eneo la kwa Mrombo katika jiji la Arusha amekuwa akitajwa kugombea ubunge wa Arusha hasa kutokana na jitihada zake kuboresha huduma za kijamii katika jiji la Arusha.