- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC ANNA MGHWIRA AMLIMA MSHAHARA MKURUGENZI
Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bi Anna Mghwira amemlima Mshahara mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva kwa kutolipwa mshahara wa mwezi Februari, 2020 hadi atakapobadilika baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu.
Bi Nghwira ametoa agizo hilo leo Ijumaa Februari 14, 2020 baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kujibu swali alilomuuliza katika kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya Mkoa huo kuhusu.
"Mkurugenzi naomba kupata taarifa ya makusanyo yenu na kiasi mlichotoa kwa vikundi vya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu, mmetoa kwa asilimia ngapi na kwa nini hamjafikia malengo kama Serikali ilivyoelekeza, β amesema Mghwira.
Baada ya swali hilo, mkurugenzi alipewa kipaza sauti ili kujibu lakini alitaka ajibu mtaalamu mwingine jambo ambalo Mghwira alilipinga na kutaka ajibu mwenyewe.
icha ya kutakiwa kujibu Lubuva alishindwa na kunyamaza kimya na kumfanya mkuu huyo wa Mkoa kumtaka mwenyekiti wa halmashauri hiyo kujibu.
Mwenyekiti wa Halmashauri, Theresia Msuya amesema kutofikia malengo kumetokana na uzembe wa watendaji.
Baada ya maelezo hayo, Mghwira alimtaka tena Lubuva kusimama na kutoa majibu kwa nini hawajafikia lengo la kutoa asilimia 10 kama Serikali inavyoelekeza lakini kwa mara ya pili alishindwa kujibu.
"Mkuu naomba radhi tugange yajayo" amesema Lubuva na kisha kuketi.
"Sasa wanaokulipa mshahara wasikulipe mwezi huu, tugange yajayo mpaka huo mwezi Machi,β amesema mkuu huyo wa Mkoa.
Mghwira amezitaka halmashauri za wilaya kuhakikisha zinatekeleza maelekezo ya Serikali ya kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya kina mama, vijana na watu wenye ulemavu.
Halmashauri ya Mwanga hadi kufikia Januari, 2020 ilikuwa imetoa Sh17 milioni kwa vikundi vya wanawake na hakuna kikundi cha vijana wala walemavu kilichopewa fedha hizo.