- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA ZAMANI WA MISRI HOSNI MUBARAK AFARIKI DUNIA
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak afariki dunia hospitalini jijini Cairo akiwa na miaka 91.
Mubarak alidumu madarakani kwa miaka 30 kabla ya kung'atuliwa jeshi baada ya maandamano makubwa ya raia.
Alikutwa na hatia ya kula njama katika mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi na kuwekwa kizuizini.
Hata hivyo, hatia hiyo iliondolewa na akaachiwa huru mwezi Machi 2017.
Kifo chake kimethibitishwa na Televisheni ya taifa ya Misri leo Jumanne. Mapema tovuti ya Al-Watan iliripoti kuwa kiongozi huyo alifariki kwenye hospitali moja ya jeshi.
Mubarak alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi Januari.
Mtoto wake wa kiume Alaa alisema siku ya Jumamosi kuwa baba yake yupo mahututi.
Baada ya kuzaliwa mwaka 1928, Mubarak aliingia jeshi kama kijana na kuendelea kuchukua jukumu muhimu katika vita kati ya Israel na Waarabu 1973.
Alikuwa rais chini ya muongo mmoja baadaye , kufuatia ,mauaji ya rais Anwar Sadat.
Alikuwa na jukumu muhimu katika mchakato wa amani wa Israel - Palestina.