November 27, 2024, 9:30 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA UTURUKI ATANGAZA KUZALISHA BANGI TENA
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, amesema nchi yake itaanza tena utaratibu wa kuzalisha bangi.
Hatua hii ya Rais Erdoğan, imekuja mara baada ya kuhudhuria kikao cha viongozi wa serikali za mitaa kilichofanyika ikulu na akufahamisha kwamba maadui wa Uturuki ambao wanajifanya ni marafiki walichukua wazo la kuzalisha bangi Uturuki na sasa hivi wanauza bangi na kujipatia kipato.
Rais Erdoğan, alisema kwamba wizara ya kilimo imeshaanza mchakato kuhusiana na suala hilo la kilimo cha bangi na kwamba Uturuki itaanza kuzalisha bangi upya.
Erdoğan, alisema katika miaka 16 ya uongozi wa chama cha haki na maendeleo (AK part) kiwango cha mfumko wa bei kimedumu katika wastani wa asilimia 9.54, kitu ambacho ni mafanikio makubwa ukilinganisha na serikali zilizopita.
Rais Erdoğan, alisema kwamba Uturuki itaingia katika hatua ambayo litakuwa ni taifa lenye nguvu na lililoendelea na kwamba kuhusiana na jambo hilo mtu yeyeto asiwe na wasiwasi.