- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA TUNISIA AFRIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 92
Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi amefariki dunia mchana wa leo Julai 25, 2019 akiwa na miaka 92, ikulu ya nchi hiyo imeeleza.
Alikuwa kiongozi mkongwe zaidi duniani. Alilazwa hospitali Jumatano lakini maafisa hawakueleza kwanini alipelekwa kupokea matibabu.
Essebsi alishinda uchaguzi huru wa kwanza Tunisia mnamo 2014 kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu.
Alilazwa hospitalini mwezi uliopita baada ya kukabiliwa na maafisa wanachotaja kuwa hali mbaya ya afya.
Waziri mkuu Youssef Chahed, aliyemtembelea hospitalini, aliwaomba watu kuacha kusambaa habari za uongo kuhusu hali yake
Mapema mwaka huu, Essebsi alitangaza kwamba hatogombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Novemba.
Aliwaambia wajumbe wa chama chake tawala Nidaa Tounes katika mkutano kwamba kijana anahitajika kuchukua uongozi. Alisema muda umewadia "kuwafungulia mlango vijana".