Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:35 pm

NEWS: RAIS WA KOREA KIM AUSHUTUMU VIKALI UWONGOZI WA MAREKANI

Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameishutumu vikali serekali ya Marekani kwa kuwa na nia mbaya kwenye mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi yake.

Image result for kim and trump summit

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Korea Kaskazini limeripoti kuwa Kim amemweleza Rais wa Urusi, VladimirPutin kwamba Marekani ilichukua msimamo wa upande mmoja kwa nia mbaya wakati wa mkutano wa kilele kati ya Kim na Rais wa Marekani, Donald Trump miezi miwli iliyopita nchini Vietnam.

Image result for kim and trump summit

Kim amekaririwa akisema amani na usalama kwenye rasi ya Korea inategemea mtazamo wa Marekani katika siku zijazo na nchi yake itajiweka tayari kwa hali yoyote itakayojitokeza.

Mkutano kati ya Kim na Trump ulivunjika bila makubaliano baada ya Marekani kusema Korea Kaskazini ilitaka kuondolewa vikwazo vya uchumi haraka bila ya kueleza iafanya nini kuhusu mpango wake wa nyuklia. Putin alitoa wito wa kulegezwa kwa vikwazo vilivyopo akisema Urusi pia inaunga mkono juhudi za kutuliza mzozo kwenye Rasi ya Korea.