Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:49 am

NEWS: RAIS WA KOREA KASKAZINI YU HAI NA ANAENDELEA VIZURI

Mshauri mkuu wa Serekali ya Korea Kusini Moon Chung-in amesema kuwa Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yupo hai na anaendelea vizuri

Mshauri huyo wa Sera za Njee wa Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameiambia CNN jumapili hii kuwa "Kim Jong Un yupo hai na waafya, yupo katika eneo la Wonsan tangu Aprili 13. Hakuna matembezi ambayo yanaonekana" amesema Kiongozi huyo wa Korea

Mwanzoni mwa weki hii CNN iliripoti kuwa intelejensia ya Marekani ilisema kuwa Afya ya Kim ni tete mara baada ya kufanyiwa upasuaji.

Tetesi za hali ya kiafya za Kiongozi huyo wa taifa lenye usiri mkubwa zaidi Duniani zilianza kusambaa, baada ya Kiongozi huyo kushindwa kuhudhuria Sherehe za Madhimisho ya Mwanzilishi wa nchi hiyo mnamo Aprili 13 mwaka huu.

Baadhi ya vyombo vya habari Duniani baada ya sintofahamu hiyo vilianza kuripoti kuwa huenda hali ya kiafya ya Kim ipo hatarini na huenda akapoteza maisha