- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA CATALONIA YUPO TAYARI KUJITENGA NA HISPANIA
Rais wa Catalonia Carles Puigdemont Siku ya Jum tano alihutubia wakazi wa Catalonia ambapo alifutilia mbali shutma za Mfalme wa Uhispania Felipe VI. Rais huyo alimkosoa Mfalme Felipe VI kwa kutotambua matakwa ya wakazi wa Catalonia baada ya kura ya maoni.
Bw Puigdemont alithibitisha nia yake ya kutekeleza matokeo ya kura ya maoni iliyopigwa siku ya Jumapili Oktoba 1. Alisema wako tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo.Katika hotuba yake ya Oktoba 4, Carles Puigdemont alishutumu mfalme wa Uhispania, ambaye aliwatuhumu viongozi wa Catalonia siku moja kabla kuhatarisha utulivu wa Uhispania nzima. "Mfalme anajikusanyia hotuba na sera za serikali ya [Mariano] Rajoy - ambazo ni hatari kuhusu Catalonia - kwa kupuuzia kwa makusudi matakwa ya maelfu ya wakazi wa Catalonia ambao hawafikiri kama wao, ambao ni waathirika wa vurugu za polisi ambazilizolaaniwa na ulimwengu mzima, "Bw Puigdemont alisema.