- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS TSHISEKEDI AKUTANA NA KABILA KUFANYA UTEUZI WAZIRI MKUU
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Antoine Felix Tshisekedi Tshilombo jana jumatatu alikutana na Mtangulizi wake Rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Joseph Kabila na kufanya mazungumzo kuhusu nafasi ya waziri mkuu ambayo imesalia wazi, miezi minne baada ya uchaguzi wa urais uliompa ushindi Felix Tshisekedi na kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.
Mazungumzo kati ya wawili hao kuhusu uteuzi wa waziri mkuu na uundwaji wa serikali yalidumu saa moja bila kupata muafaka juu ya kumpaka waziri mkuu huyo ajaye.
Kuhusu swala la waziri mkuu, mazungumzo yanaendelea, karibu miezi minne baada ya Felix Tshisekedi kuapishwa kama Rais wa Jamhuri. Mwanzoni, wawili hao walikuwa wamechagua timu za mazungumzo, lakini mazungumzo yao yaliambulia patupu. Mazungumzo sasa yanafanyika katika ngazi ya juu.
Wananchi wa Congo wanaendelea kusubiri kwa hamu na gamu uteuzi wa waziri mkuu mpya, miezi kadhaa tangu Felix Tshisekedi Tshilombo kuchukuwa mikoba ya Joseph kabila Kabange kwenye uongozi wa nchi.
Awali Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikuwa hawaelewani kufuatia mvutano wa kisiasa uliokuwa iliikumba DRC na kisha baada ya uchaguzi wa urais wawaili hao waliamua kufanya kazi kwa ushirikiano wakiwa katika muungano mmoja wa kisiasa.
Rais Tshisekedi na Joseph Kabila walikuwa hawajakutana kwa wiki kadhaa kutokana na ziara za kikazi za Tshisekedi. Lakini kwa pande zote mbili, wanahakikisha kuwa rais wa sasa na mtangulizi wake huzungumza mara kwa mara.