Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:44 am

NEWS: RAIS TRUMP ASHTAKIWA KATIKA MAHAKAMA YA CALIFORNIA

U.S.A: Muungano wa zaidi ya majimbo 15 nchini Marekani yakiongozwa na jimbo la California yamemshitaki Rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusu uamuzi wake wa kutangaza hali ya dharura ili kukusanya fedha kwa niaba ya ujenzi wa ukuta wa mpakani na Mexico.

Kesi hiyo imewasilishwa katika mahakama ya wilaya ya kaskazini katika jimbo la California.

Hatua ya wananchi hao Inajiri siku kadhaa baada ya Trump kuidhinisha hali ya dharura, inayompa nguvu kulivuka bunge na kujipatia fedha kwa ujenzi huo - ambayo ni ahadi kubwa aliyotoa wakati wa kampeni yake.

Ujenzi huo umekuwa ukipingwa na wananchi wengi nchini Marekani hata chama cha Democrats kimeapa kupinga hatua hiyo "kwa kutumia njia zozote zilizopo".

Mkuu wa sheria katika jimbo hilo la California Xavier Becerra amesema wanampeleka Trump mahakamani "kuzuia matumizi mabaya ya nguvu za rais".

"Tunamshtaki Trump kumzuia dhidi ya kuiba pesa za mlipa ushuru, zilizotengwa kisheria na bunge kwa watu wa majimbo yetu. Kwa wengi wetu, ofisi ya rais sio eneo la vioja ," aliongeza

Kesi hiyo iliyowasilishwa Jumatatu inaanza kwa kusikizwa awali ombi la kutaka kumzuia Trump ashughulikie dharura hiyo aliyoitangaza, wakati kesi ikiendelea kotini, gazeti la Washington Post linaripoti.