Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:45 am

NEWS: RAIS TRUMP ALALAMIKIA UWAMUZI WA KUMUONDOA MADARAKANI

Rais wa Marekani Donald Trump amewalalamikia na kuwashutumu vikali viongozi wa wanademokratiki katika bunge la wawakilishi nchini humo kwa kushindwa kuwasilisha kwa baraza la seneti mashitaka mawili yanayolenga kumuondoa madarakani kwa madai ya kutumia vibaya madaraka na kukataa kutoa ushirikiano kwa bunge wakati wa uchunguzi dhidi yake.

Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi amesema kwanza anataka kuelezwa masharti ambayo Bwana Trump atashitakiwa nayo kabla ya kutuma mashitaka hayo kwa baraza la seneti.

Wanasiasa waandamizi wa chama cha Trump cha Republican katika baraza la seneti ambao ndiyo wenye wingi wa viti wamesema wako tayari kushirikiana na Ikulu ya Rais kuhakikisha Rais Trump anaondolewa mashitaka hayo haraka iwezekanavyo.

Bunge la Wawakilishi (Kongresi) lilipigia kura mashtaka mawili - kwamba rais alitumia vibaya mamlaka yake na kwamba alizuia shughuli za Bunge hilo.

Kura zote zilipigwa kulingana na mirengo ya vyama huku karibu wabunge wote wa chama cha Democtrats wakipiga kura kuunga mkono ashtakiwe huku Republican wakipinga kura hiyo.

Wakati kura ilipokua inapigwa, Bwana Trump alikuwa akihutubia mkutano wa wafuasi wake.

Mashtaka mawili aliyoshutumiwa nayo rais ni utumiaji vibaya wa mamlaka yake na kwamba alizuia shughuli za Bunge hilo.