Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:48 pm

NEWS: RAIS TRUMP AKWEPA KASHFA YA KUSAIDIWA NA URUSI UCHAGUZI MKUU

Ripoti ya Mwanasheria Maalum anayehusika na uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani imebaini kwamba hakuna njama yoyote kati ya timu ya Donald Trump na Urusi kuhusu uchaguzi wa Marekani, uliompelekea rais huyo kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Waziri wa Sheria wa Marekani Bill Barr amewasilisha kwenye bunge la Congress muhtasari wa ripoti ya Mwanasheria Maalum Robert Mueller kuhusu uchunguzi wa madai ya ushirikiano kati Urusi na timu ya kampeni ya Donald Trump mnamo mwaka 2016.

Kwa upande wa ikulu ya White House , kesi hiyo imeweka wazi kuwa rais Donald Trump "amesafishwa" na "hakuhusika na njama na Urusi."

Mwendesha mashtaka Robert Mueller ametoa uamuzi huo baada ya karibu miaka miwili ya uchunguzi.

Ripoti yake iliwasilishwa kwa Waziri wa Sheria siku ya Ijumaa. Siku ya Jumapili Machi 24 Waziri Bill Barr alitoa muhtasari wa kura nne. kwa maneneo machache, alimsafisha rais wa Marekani na timu yake kwa kutohusika na njama yoyote na Urusi wakati wa kampeni ya uchaguzi ya mwaka 2016.