- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS PETER MUTHARIKA ASHINDA URAIS KWA USHINDI MWEMBAMBA
Rais wa Malawi Peter Mutharika amechaguliwa kwa muhula wa pili madarakani kuliongoza taifa la Malawi kwa idadi ndogo sana ya Kura ya asilimia 38.6% baada ya kupata ushindi katika uchaguzi wa wiki iliyopita uliogubikwa na madai lukuki ya udanganyifu.
mpinzani wake wa karibu Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress MCP amepata asilimia 35.4 ya kura zote.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jane Ansah alietangaza matokeo hayo alisema kuwa, "ninapenda kutanguliza pongezi zangu kwa rais mteule na makamu wake. Umechaguliwa na watu wa Malawi kuiongoza nchi kuelekea mustakabali bora, umepewa jukumu la kuongoza ajenda ya maendeleo ya taifa hili kwa miaka mitano ijayo."
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo uliofanyika wiki iliyopita yalitangazwa baada ya kuzozaniwa mahakamani ambapo kiongozi wa upinzani Chakwera alipata zuio la muda la mahakama kutokana na madai ya udanganyifu.
Jaji wa mahakama kuu Charles Mkandawire aliondoa zuio hilo na dakika chache tu baadae tume ikathibitisha ushindi wa Mutharika. Chama cha upinzani cha MCP kiliitaka tume ya uchaguzi kuchunguza madai 147 yaliyowasilishwa kuhusiana na hitilafu zilizojitokeza wakati wa uchaguzi. Mahakama baadae ilisema kwamba uchunguzi kuhusiana na madai ya udanganyifu unaweza kuendelea baada ya matokeo kutangazwa.
Vyama vya upinzani vimelalamika kwamba idadi kubwa ya karatasi za kupigia kura zilikuwa zimechezewa kwa kutumia wino wa kufanya masahihisho. Mkuu wa jeshi la polisi Rodney Jose ametoa onyo kali dhidi ya waandamanaji wa upinzani ambao walijitokeza katika mji mkuu wa Lilongwe na mji wa kaskazini wa Mzuzu akisema ghasia hazitavumiliwa.
Waangalizi wa Umoja wa Ulaya walielezea kampeni za uchaguzi kuwa "ziliandaliwa vyema, zilishirikisha wote na zilikuwa za wazi na zenye ushindani".