- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS OMAR AL BASHIRU WA SUDAN APINDULIWA NA JESHI LA NCHI HIYO
RAIS wa Sudan Omar al-Bashir anaonekana ameondolewa madarakani na Jeshi la Nchi Hiyo baada ya Ikulu yake kuzingirwa na jeshi la nchi hiyo na Imeripotiwa kuwa maofisa kadhaa wa serikali, wakiwamo mawaziri wamekamatwa na Uwanja wa ndege jijini Khartoum umefungwa.
Magari ya kijeshi ya Sudan yametumwa leo Alhamisi asubuhi kwenye madaraja ya Mto Nile na katika maeneo kuu ya mji mkuu, Khartoum, ambapo watu wameonekana wakiimba "amenguka, tumeshinda!" wakimaanisha rais Omar al-Bashir, mwandishi wa shirika la Habari la Reuters ameripoti.
Maelfu ya watu wameungana na wenzao wanaokusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi tangu mwanzoni mwa wiki hii, kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters.
Mapema asubuhi, televisheni ya taifa imeripoti kuwa jeshi linajiandaa kutoa tangazo muhimu. Kituo hicho cha serikali kimekuwa kikirusha nyimbo za kizalendo, na hivo kuchochea uvumi kwamba Omar al Bashir ameanza kushinikizwa kuachia ngazi.
Rais Omar al-Bashir ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1989 anakabiliwa na maandamano tangu mwezi Desemba mwaka jana ya kumtaka ajiuzulu.