- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS NYUSI ASHINDA UCHAGUZI WA URAISI
Tume ya uchaguzi nchini msumbiji-CNE imemtangaza Rais wa Msumbiji aliyepo madarakani Philipe Nyusi ameshinda uchaguzi kwa asilimia 73 ya kura katika uchaguzi wa urais na kuchukua ushindi mkubwa huku vyama vya upinzani vinasema uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura pamoja na ghasia.
Mgombea wa chama kikuu cha upinzani, Ossufo Momade na pia mwanachama wa zamani wa kundi la waasi la Renamo ameshikilia nafasi ya pili kwa kupata asilimia 21.88 ya kura, alisema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo Abdul Carimo kwenye mkutano wa Jumapili na waandishi wa habari.
Rais Nyusi kutoka chama tawala cha Frelimo alisema katika muhula wake wa pili madarakani kwa miaka mitano atakuwa na jukumu kubwa kuangalia uzalishaji gesi ya asili unaoongozwa na makampuni makubwa ya mafuta kama vile Exxon Mobil Corp na Total, kupambana na uasi wenye itikadi kali ya ki-Islam na kutekeleza mkataba wa Amani uliotiwa saini miezi miwili iliyopita.