- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS NKURUNZIZA AFANYA ZIARA YA KWANZA NJE YA NCHI TANGU 2015
KAGERA: Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amefanya ziara ya kushtukiza njee ya nchi yake, na hii inakuwa ni ziara yake ya kwanza tangu kutokea jaribio la kumwondoa madarakani mwaka 2015. Nkurunziza amezuru nchini Tanzania katika Wilaya ya Ngara, kukutana na mwenyeji wake rais John Magufuli.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara
Ziara hii imekuja wakati huu Tanzania ikiendelea kutoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi 200,000 waliokimbia nchi yao kwa sababu za kiusalama.
Rais Nkurunziza ameandamana na idadi kubwa ya Mawaziri wake katika ziara hiyo ya kwanza ambayo ilitangazwa katika dakika za lala salama.
Jaribio la kumpindua Nkurunziza lilifanyika wakati akihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiwahotubia wananchi, rais Nkurunziza amewaambia wakimbizi wanaoishi nchini Tanzania kurejea nyumbani ili kuijenga nchi yao.
"Tunawaomba raia wa Burundi wanaoishi hapa nchini Tanzania, kurudi nyumbani ili tuijenge nchi yetu," alisema.
Aidha, ameishukuru Tanzania kwa kuwa jirani mwema na kuwapa hifadhi raia wa Burundi waliokimbia nchi yao.
Rais Magufuli amesisitiza ujumbe wa rais Nkurunziza na kuwataka wakimbizi hao kuchukua hatua za kurudi nyumbani kwa hiari.
"Rudini nyumbani kwa hiari, sisi hatutawafukuza," alisema rais Magufuli.
Mamia ya watu wamepoteza maisha na wengine kutoweka kwa mujibu wa Mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za Binadamu kama Human Rights Watch.
Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa ni mratibu wa mazugumzo ya kisiasa nchini humo, ambaye ameendelea kujaribu kuwaleta wapinzani wa kisiasa nchini humo kujaribu kuleta mwafaka wa kisiasa nchini humo.
Hata hivyo, kumekuwa na changamoto ya kuwakutanisha wanasiasa wa upinzani na viongozi wa serikali.