- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS NKURUNZINZA ATOA KAULI YA KUTOGOMBEA MWAKA 2020
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa mara nyingine tena ametoa msimamo wake wa kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.Hatua ambayo imeonekana kuwashangaza raia wengi wa Burundi huku wapinzani wake wakijiuliza ikiwa kauli yake itakuwa na ukweli.
Rais Nkurunziza ameyasema hayo mwishoni mwa juma mbele ya maafisa wa jeshi na polisi kwenye sherehe zilizokuwa zimeandaliwa na taasisi hizo kumtakia siku kuu njema za mwisho wa mwaka.
Hatua hii inakuja wakati huu kukiwa na uvumi kwamba kiongozi huyo wa taifa la Burundi ana nia ya kuwania kiti cha uraisi katika uchaguzi ujao.
Burundi inaingia mwaka 2020 ikiwa na kumbukumbu ya visa vya mauaji na mivutano ya kisiasa vilivyoshuhudiwa mwaka 2019 ikiwa imesalia miezi kadhaa kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais nchini humo.
Visa vya kuteketezwa kwa moto ofisi ndogo za chama kikuu cha upinzani cha CNL, katika maeneo mbalimbali ya nchi vilishuhudiwa, huku chama hicho kikinyooshea kidole cha lawama vijana kutoka chama tawala, CNDD-FDD, Imbonerakure kuhusika na visa hivyo.