- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MUSEVENI AWEKA MARUFUKU YA KUTOTOKA NJEE
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti mapya katika nchini hiyo ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona, hii ni wiki mbili tu baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.
Katika hotuba yake iliyorushwa kwenye televisheni usiku wa jana Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.
Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani
Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .
Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.
Bw. Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''
Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Magari binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. Limeandika gazeti la New vision la Uganda.
''Isipokuwa kwa ndege za mizigo, malori, magari aina ya pickups na treni, kuanzia siku ya Jumanne tarehe 31 mwezi Machi saa moja, amri ya kutotoka nje itatekelezwa katika nchi yote ya Uganda'' Meseveni aliesema.
Alisema kuwa siku 14 zitatumika kubaini na kuwafuatilia na kuwatenga wale wote waliokaribiana na watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.