- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MUSEVENI AJITETEA KWA RAIS KAGAME MADAI YA KUONGEA NA WAASI WAKE
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameamua kuwa muwazi juu ya madai ya kukutana na mfanyibiashara, raia wa Rwanda Tribert Rujugiro Ayabatwa, ambaye pia ndio mpinzani mkuu wa Rais Kagame pia inaelezwa kuwa yeye ndiye chanzo cha mvutano kati ya mataifa hayo mawili jirani.
Kupitia barua aliyomwandikia rais wa Rwanda Paul Kagame, tarehe 10 mwezi huu na kuchapishwa katika Gazeti la serikali New Vision, siku ya Jumanne, rais Museveni ameelezea mazingira aliyokutana na mfanyibishara huyo ambaye Rwanda inasema, yeye na wengine ni waasi wanaopanga kuiangusha serikali yake.
Katika barua hiyo, rais Museveni anamwambia rais Kagame kuwa, alikataa kutoa uungwaji mkono kwa mfanyibiashara huyo, ambaye alikuwa anamwelezea mambo ya ndani ya Rwanda, na akamweleza kuwa msimamo wa Umoja wa Afrika ni kwamba, nchi nyingine haiwezi kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.
Aidha, Museveni ameeleza kuwa alikutana na mfanyabiashara mwingine Bi.Charlotte Mukankusi ambaye alimwomba msaada baada ya kudai kuwa serikali ya rais Kagame ilikuwa imemuua mume wake.
Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa barua hii inaonesha kuwa, kuna zaidi ya mvutano wa masuala ya kibiashara wakati huu ufumbuzi ukiwa bado haujapatikana
Serikali ya Rwanda imekuwa ikiishtumu Uganda kwa kuwapa hifadhi na kuwaunga mkono wafuasi wa vuguvugu la RNC, ambalo Kigali inasema ni maadui wa serikali.