- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MUGABE ALIFARIKI KWA UGONJWA WA TEZI DUME
Taarifa kutoka nchini Zimbabwe zinasema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bw Robert Mugabe, alikuwa anasumbuliwa na saratani ya Tezi Dume, iliyosababisha kifo, mapema mwezi huu nchini Singapore.
Gazeti linalofadhiliwa na serikali nchini humo The Herald, limeripoti kuwa licha ya Mugabe kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu, afya yake ilianza kuwa mbaya baada ya kuondolewa madarakani na jeshi mwaka 2017.
Wakati wa uhai wake, Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa anakwenda mara kwa mara kupata matibabu nchini Singapore wakati huo, ikishukiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na saratani ya tezi dume.
Rais Emmerson Mnangagwa akiwa jijini New York amenukuliwa na Gazeti la The Herald akiwaambia wafausi wa chama cha ZANU PF kuwa, madaktari walishindwa kuendelea kumpa matibabu Mugabe kwa sababu ya umri wake mkubwa lakini pia saratani ilikuwa imesambaa sana mwili na hivyo, matibabu yalikuwa hayasaidii.
Mugabe aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 37, anatarajiwa kuzikwa mwezi ujao katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.