- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MPYA WA TLS AAHIDI KUPIGANIA UTAWALA WA SHERIA
Rais mteule wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Dk. Rugemeleza Nshala amesema ataendelea kupigania utawala wa sheria na kutekeleza matakwa ya TLS.
Alisema mbali ya kupigania utawala pia TLS itaendelea kuhakikisha wanachama wake wanapata mafunzo mazuri ya sheria.
“Tutahakikisha tunaendeleza wanachama wetu kupata elimu na kufanya kazi zao bila matatizo.
“Mawakili au Wanasheria wafanye kazi zao kwa uhuru bila kunyanyaswa, kutishwa na kuwekwa ndani ambako kumejitokeza hivi sasa.
“Mawakili ni watu muhimu katika kuhakikisha nchi inatawaliwa chini ya utawala wa sheria kama Katiba inavyosema,” alisema Dk. Nshala.
Jana kwenye uchaguzi wa chama hicho Nasha alipata kura 647 ambazo ni mara mbili ya wapinzani wake.
Akitangaza matokeo hayo jana kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Bahame Nyanduga alisema jumla ya kura 1,227 zilipigwa.
Alisema wagombea wa nafasi ya urais walikuwa; John Sekka aliyepata kura 29, Gasper Nicodemus kura 58, Godfrey Wasonga kura 123, Godwin Ngwilimi kura 354 na Dk. Rugemeleza Nshala kura 647.
“Kwa niaba ya Kamati ya uchaguzi na mtangaza rasmi Dk. Nshala kuwa Rais mpya wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika TLS kwakupata kura 647,”alisema Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Nyanduga.