Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 2:30 am

NEWS: RAIS MPYA WA CONGO ASHINDWA KUUNDA SEREKALI MPYA KWA WIKI YA 4

Tafsiri ya moja kwa moja inaonesha kwamba Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bw Felix Tshisekedi Tshilombo ameshindwa kuunda baraza jipya la Mawaziri na mpaka sasa ni wiki ya nne tangu kutawazwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo na hajafanya teuzi yeyote tangu aingia madarakani baada ya Rais wa muda mrefu Joseph Kabila kutoka katika kiti hicho.

Ripoti kutoka nchini Congo humo zinaonesha kuwa Mawaziri mbalimbali wa serikali iliyokuepo wameanza kujiuzulu mmoja baada ya mwengine licha ya Bunge la taifa kutoa nafasi kwa mawaziri hao hadi usiku wa manane kuwataka kuendelea kuhudumu katika serikali au kushiriki katika bunge.

Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa rais mpya wa DRC, Felix Tshisekedi Tshilombo, ameshindwa kuunda serikali kutokana na mgawanyiko unaoikumba jamii ya wanasiasa nchini humo.

Related image

Wakati huo huo Waziri Mkuu Bruno Tshibala hajajiuzulu kwenye nafasi yake wala kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa serikali yake, jambo ambalo hata hivyo, aliombwa kufanya. Mawaziri mbalimbali na wabunge wamelazimika kila mmoja kujiuzulu kwenye nafasi zao.

Lakini kujiuzulu haimaanishi kuachia ngazi . "Huwezi kuachia ngazi kabla ya kukabidhiana madaraka na warithi wetu," amesema msemaji wa serikali inayomaliza muda wake, ambaye hata hivyo, amekumbusha kwamba yeye na mawaziri wenzake wanaendelea kuratibu shughuli ndogo ndogo za serikali.

Kwa upande wa uundwaji wa serikali, kazi kubwa iko mikononi mwa rais mpya Felix Tshisekedi, kwa vile ni rais ambaye anatakiwa kuteua waziri mkuu kutoka kambi ya walio wengi bungeni.

Wengi wameendelea kukosoa kuchelewa kutangazwa kwa serikali mpya.