- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULIA AWAPIGA MARUFUKU WENYE MAJINA YA WAGOMBEA MFUKONI
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli amewataka viongozi wote wa mikoa na wilaya wa chama hicho kutokuwa na majina yao mfukoni katika kipndi cha mchakato wa kura ya maoni kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge wanaokiwakisha chama kwenye Chaguzi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi wa mikoa, wilaya na jumuiya za chama hicho kutoka mikoa yote nchini.
Amewataka viongozi hao kuweka mbele maslahi ya chama hicho kwa kuchagua wagombea wenye sifa na wanaokubalika kwa wananchi.
Amesema ndani ya CCM, kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
"Wakati wa mchakato wa uchaguzi, tusiende na majina mfukoni, kwamba huyu ni wa mwenyekiti, huyu ni wa katibu. Wakati mwingine unakuta mwenyekiti na katibu mkuu wanagombana. Tuweke maslahi ya chama chetu mbele," amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema chama hicho kiko imara, viongozi wasibabaishwe na kelele ndogo za washindani wao ambao nguvu zao zimekwisha.
"Tuache kugombana hasa kwenye nafasi za ubunge na udiwani. Wakati mwingine tunawapoteza wagombea wazuri mpaka wanahama, mambo haya hayatatokea tena," amesema mwenyekiti huyo wa CCM.