Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:41 am

News: Rais Magufuli walioko tayari kuyeya kenya kusomea udaktari safari imewadia.

Dodoma: Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh,John pombe magufuli ameagiza madaktari 258 ambao walikuwa tayari na wamekidhi vigezo kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nchini kenya kupatiwa ajira hapa nchini mara moja.

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto mh,Ummy Mwalimu ameyabainisha hayo leo wakati akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa idara ya habari uliyopo bungeni mjini dodoma.

Ambapo amesema kuwa rais amefikia uamuzi huo baada ya mahakama nchini kenya kuweka pingamizi kwa serikali ya kenya kuendelea na mchakato wa kuajiri madaktari 500 kutoka nchini tanzania,hivyo kwa kuwa madaktari hao wameonyesha utayari wa kufanya kazi katika mazingira yoyote .


Mh.Mwalimu ameongeza kuwa wizara ilipokea maombi 496 na baada ya kuyachambua madaktari 258 ndiyo waliokidhi vigezo vilivyokuwa vimewekwa,pamoja na hayo amesema kuwa bado tanzania ipo tayari kuipatia nchi ya kenya madaktari wengine pindi wakiwahitaji.


Wakati huo huo katibu mkuu wizara ya afya dk ulisubisye mpoki amewatoa hofu watanzania juu ya ugonjwa wa amofilia kwa kusema kuwa ugonjwa huo si wa ajabu na mpya kama wengi wanavyodhani bali ni ugonjwa wa hatari kwani ni wa kurithi ambao husababisha shida katika damu kuganda na kuwa wapo wataalumu wengi amabao wanaweza kushughulikia tatizo hilo.

kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko juu ya upungufu wa wataalamu wa afya katika vituo vya afya hasa katika vituo vya afya vilivyoko maeneo ya vijijini hivyo kuajiriwa kwa madaktari 258 kutasaidia kupunguza tatizo hilo