- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI : WAHUJUMU UCHUMI 138 WAMERUDISHA MABI
Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli amesema watuhumiwa 138 wenye mashtaka ya uhujumu uchumi waliomba msamaha kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) wamesharudisha mabilioni ya fedha huku nyaraka za watuhumiwa wengine 500 zikiendelea kuchambuliwa.
Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 mjini Mpanda wakati akizindua safari za ndege kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Katavi.
“Leo nilikuwa nazungumza na DPP kuhusu taarifa za watu waliotubu. Mpaka leo wamefikia 138, wamesharudisha baadhi ya mabilioni ya fedha,” amesema Rais Magufuli. “Walioachiwa wako huru wamekwenda kujumuika na familia zao.
''Huo ndiyo upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha na wao wamepokea na sisi tunashukuru. Hao sasa ni raia wema wahesabike kuwa ni raia wema katika nchi yetu.” “Nao wataendelea kuachiwa kadri watakavyokuwa wakirudisha fedha, hizo fedha zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.” amesema Rais Magufuli
Amesema kulikuwa na watuhumiwa 700 walioomba msamaha lakini wanaendelea kuchambua mmoja baada ya mwingine.
Raisi Magufuli 22 Septemba 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam alishauri mahabusu wa makosa mbalimbali hasa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ambao wapo tayari kuomba msamaha na kurudisha fedha walizotakatisha, wasikilizwe na Ofisi ya DPP ndani ya siku saba kuanzia Jumatatu Septemba 23 hadi Jumamosi ya Septemba 28, 2019.
Kiongozi huyo wa Tanzania amerejea kauli aliyowahi kuitoa huko nyuma kwamba hapendi kuongoza taifa la watu wenye machungu hususan waliopo magerezani huku akitamani siku moja kusiwe na mahabusu wala wafungwa. “Mimi naumia kuona watu wapo mahabusu au watu wamefungwa. Ni bahati mbaya kwa sababu sheria zipo. Lakini mtu anapowekwa mahabusu inaumiza sana,” amesema Magufuli.
“Najua wanateseka, unawaona wanavyopelekwa mahakamani, wengine wamekonda kweli inatia huruma inaumiza. Najua wengine wanataka kuomba msamaha waje kwako DPP mpange warudishe,” amesema Magufuli