- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI LEO AMEMUAPISHA NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI NA MABALOZI
Dar es salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2017 amemuapisha Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - anayeshughulikia Elimu.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Tixon Tunyangine Nzunda kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI
Viongozi wengine walioapishwa na Mhe.Rais Dkt. Magufuli ni Bwa. Rajab Omar Luhwavi ambaye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.
Pia Rais Magufuli amemuapisha Bw. Bernard Mtandi Makali ameapishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na Bw. Clifford Katondo Tandari, kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Rajab Omar Luhwazi kuwa Balozi nchini Msumbiji
Mwingine aliye apishwa leo na Rais Magufuli Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).Viongozi wote walioapishwa wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hafla ya kuapishwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Hapa watumishi wakila kiapo