- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: RAIS MAGUFULI AZINDUA MABWENI MAPYA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Dar es salaam, Mh. Dkt John Pombe Magufuli ambaye ni raisi wa Tanzania, amehutubia hafla ya uzinduzi wa mabweni mapya katika chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kama Mlimani. Mabweni hayo ni moja ya matunda ya kujivunia katika serikali ya awamu ya tano. ikiwa yaliwekewa jiwe la msingi na pia kuzinduliwa na raisi wa awamu hii.
Mh. Raisi akizindua ujenzi wa mabweni hayo.
Katika tukio hili la kihistoria raisi kabla ya hotuba aliwaomba watanzania wote waliofika katika eneo hilo kusimama kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kuwaombea dua na heshima kwa askari 8 waliopoteza maisha mkoani Pwani. Raisi ameendelea kuuthibitishia umma wa kitanzania kwamba nchi inaweza kufikia malengo yake ya kimaendeleo bila kutegemea msaada wa nje na pia kwa kutumia wataalam na wakandarasi wazalendo.Ujenzi wa mabweni hayo umekamilika kwa kipindi kifupi hali ya kuwa na ubora wa juu na gharama zikiwa ni za chini kabisa.
Mh Raisi na waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh joyce ndalichako akiakagua ujenzi na wakandarasi wazawa wakiwa kazini
Maneno aliyoyasema raisi katika hotuba yake ni haya, "mabweni ya mabibo yalijengwa miaka ya 2000 kwa shilingi bilioni 27 na yanachukua wanafunzi 4000. haya yamejengwa sasa kwa biloni 10 tu na yanachukuwa wanafunzi 3840". mabweni haya yameonekana kuwa na tija zaidi kwa wadau wa chuo hicho hasa wanafunzi na wazazi wao, kwakuwa yamejengwa karibu na chuo hicho llakini pia ubora zaidi, huku serikali ikifaidika na matumizi madogo kigharama.