- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWAUMBUA TRA, ASEMA WAMEHUSIKA KUIBA BILIONI 10
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ameibua kashfa mpya na nzito juu ya Mamlaka yenye dhana ya ukusanyaji mapato nchini Tanzania (TRA), akisema wahujumu uchumi wamewahi kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutengeneza stampu hewa zenye thamani ya Sh10 bilioni.
Amesema stampu hizo baada ya kutengenezwa zilisambazwa katika viwanda nchini kupitia ushirikiano wa baadhi ya wafanyakazi wa TRA.
“Kwenye suala hili la kodi hasa kwenye vinywaji kama vile bia, konyagi na spirit (vinywaji vikali) nyingine hili kidogo ni very complex (linachanganya) ndio maana mwenyekiti hakuzungumza tulikuwa tunakusanya kiasi gani, angezungumza hilo tungekuwa tunagonga stampu tungekuwa tunakusanya ngapi, tungepata jibu vizuri.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne Aprili 9, 2019 akifungua kiwanda cha majani ya Chai katika kijiji cha Kabambe mkoani Njombe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye mikoa mbalimbali nchini.
“Hatukusanyi kitu katika eneo ambalo tumepigwa sana ni hilo la vinywaji, kwa hiyo Serikali inakosa pesa hakuna mahali tulipata pesa, lazima sasa tutafute utaratibu mzuri ili hawa wenye viwanda vya vinywaji tusipoteze pesa zaidi,” amesema Rais Magufuli.