- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWATAKA MA-DC KUACHA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA
Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya wote kuacha kutumia madaraka yao vibaya na mamlaka walizopewa ikiwamo za kuweka watu ndani na kuwatoa wakidai wamejifunza bila kupelekwa mahakamani.
Kauli hiyo ya Rais Magufuli ameitoa leo wakati wa kuwaapisha majaji 15 wa Mahakama Kuu na 6 wa Mahakama ya Rufani.
Rais Magufuli amesema kama mkuu wa wilaya ana mamlaka hayo ya kumuweka ndani na mkuu wa mkoa akiamua kuweka watu ndani itakuwa ni vurugu, huku akibainisha kuwa mambo mengine yanahitaji kutolewa maelekezo tu.
“Kuelekeza kunaweza kuwa na matokeo chanya wakati mwingine kuliko hata kuweka watu ndani,” amesema. Magufuli Magufuli amesema ameamua kumtoa katika uongozi aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho na kumhamishia katika kitengo cha wadudu kwa sababu yeye ni mtaalamu wa eneo hilo.
Amesema yaliyokuwa yakitokea wilaya ya Mwanga ya kuwaweka watendaji wa Serikali ndani akiwamo katibu tawala, mkurugenzi kila mmoja alikuwa akiyaona huku vurugu zote zilikuwa zikianzia kwa kiongozi huyo. “Hata katika mazungumzo yake amekuwa akisema yeye ni mtaalamu pekee wa wadudu Tanzania hakuna kama yeye hivyo nikaamua kumpeleka huko huenda atafanya vizuri...” amesema Magufuli.
Akizungumzia wilaya ya Tarime Rais Magufuli amesema kuna changamoto nyingi ndiyo maana aliamua kumuweka (Charles Kabeho aliyekuwa kiongozi wa mbio za mwenye mwaka 2018) kwa sababu alikuwa akiona jinsi anavyokemea mabaya na kukataa rushwa.