- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWASIMAMISHA KAZI WAHANDISI 12 MOROGORO
Rais Dk John Magufuli amewasimamisha kazi wahandisi kumi na wawili wa ofisi ya wakala wa barabara mkoa wa Morogoro TANROADS mara baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wao katika daraja la Mkange Kiyegeya wilayani Kilosa.
Uwamuzi huo wa Rais Magufuli ameutoa leo Machi 16, 2020 mara baada ya kufanya ziara katika Daraja hilo na kukundua kuwepo kwa uzembe mkubwa wa watendaji wa TANROADS na Watendaji wa Wizara.
Pia Rais Magufuli ametoa onyo la Mwisho Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi Mhandisi Isaack Kamwelwe sambamba na Mtendaji Mkuu wa matengenezo Mhandisi Mohamed Ntandu kutokana na kutofuatilia utendaji wa mkoa katika ukaguzi wa barabara baada ya mkoa kupatiwa zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kazi hiyo na kuwasamehe Mtendaji Mkuu TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale.
Daraja la Kiyegeya limekuwa ni nguzo muhimu kwa kuwaunganisha wakazi wa Morogoro na Jiji la Dodoma likukuwa kwenye ukarabati tangu kusombwa na Maji.