- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWAONYA WANAOPANDISHA BEI YA VITU MWEZI MTUKUFU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaonya vikali wale wote wenye tamaa za kupandisha bei ya vyakula wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhan, nakuwataka watu hao kuacha tabia hiyo mara moja.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumapili ya Mei 19, 2019 katika Mashindano ya 20 ya kusoma na kuhifadhi Quran Afrika yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Amesema kufanya hivyo ni dhambi mbele ya mwenyezi Mungua kufanya hivyo hakuwezi kumtajirisha mtu hasa kwa kupandisha bei ya vile vitu vinavyotumika sana katika mfungo huu.
“Nitumie fursa hii kutoa wito kwa Mamlaka husika za serikali kufuatilia suala hili kwa ukaribu sana.” Amesema Magufuli Mbali na hilo amewataka watu wa madhehebu mengine na wale wasiokuwa na dini kuendelea kushirikiana na Waislamu katika kutimiza mfungo wa mwezi huu ambao ni moja kati ya nguzo tano za Uislamu.
“namuomba Mungu awalipe malipo stahiki juu ya kile mnachokifanya katika funga zenu, Mimi mwenyewe sijafunga lakini siku ya kufumgua waislamu ntakua nanyi katika pilau.” Amesema Magufuli.