- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA REGINALD MENGI
Dar es Salaam: Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewaongoza Watanzania waombolezaji katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi aliyefaiki nchini Dubai.
Mengi ameagwa leo Jumanne Mei 7, 2019,na Rais Magufuli pamoja na viongozi wengine waliohudhuria akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, viongozi wastaafu, viongozi wa dini, kisiasa na watu mbalimbali.
Pia alikuwepo SheIkh wa Mkoa wa Dar es Salaama, Alhad Musa Salum ambaye amewataka Watanzania kumuenzi Mengi kwa vitendo kutokana na mambo mema aliyoyafanya kwenye jamii wakati wa uhai wake.
Reginald Mengi alifariki usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 akiwa Dubai, Falme za Kiarabu.
Amemtaja Mengi kama muasisi wa kamati za amani za mikoa na siku zote alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha amani, upendo na utulivu vinaendelea kutawala.
Naye Askofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Nelson Kisare amewataka viongozi kutumia nafasi walizonazo kubadili maisha ya Watanzania kwa kutumia rasilimali zilizopo Tanzania
Pia kwa upande wa Mkurugenzi wa Clouds Media Joseph Kusaga amesema "Mimi nimemjua miaka 22 iliyopita nikiwa napiga party nyumbani kwa Mzee Mengi. Tulikuwa tunaongea mambo ya Redio, yeye akaanza na mimi nikaendelea kuchukua ujuzi. Imagine mtu ana kituo cha redio halafu anakupa ujuzi wa kufungua Redio!... Imagine."