- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AUZUNGUMZIA UCHAGUZI WA SEREKALI ZA MITAA
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amewataka Watanzania kutumia uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba mwaka 2019 kuchagua viongozi watakaozingatia maadili na kumshauri vyema yeye ili kuwaletea maendeleo.
Oktoba mwaka 2019, Tanzania itafanya uchaguzi wa serikali za mitaa
Magufuli ametoa wito huo leo Jumatatu Julai 15,2019 wakati akizungumza na wananchi wa Katoro na Buselesele mkoani Geita akiwa njiani kuelekea Magogo Geita ambako atazindua nyumba za askari wa jeshi la polisi.
“Mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, chagueni viongozi wazuri, msichague viongozi wanaowapa rushwa, mkikosea kuchagua madhara yake ni makubwa.” “Mkasimame imara katika kuchagua viongozi ambao mnafikiri wataweza kunisaidia pia na kunishauri vizuri,” amesema
Rais Magufuli pia amesisitiza wakazi wa maeneo hayo kudumisha amani, upendo na umoja na kutokubali kufarakanishwa. “Msikubali watu kuwatofautisha, endelezeni misingi ya amani na umoja aliotuachia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,” amesema