- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,973
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 Katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano ambapo kati yake wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao, na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.
Msamaha huo ameutoa leo Aprili 25, 2020 katika taarifa yake ya kuwatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mhe. Rais Magufuli amesema ana matumaini kuwa wafungwa haowamejifunza na watajirekebisha ili waungane na jamii katika kulitumikia Taifa wakiwa raia wema wanaozingatia sheria na taratibu.
Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kutumia siku ya kesho (26 Aprili, 2020) kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa wa Corona.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona (Covid-19) ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko na safari zisizo za lazima.