Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:20 am

NEWS: RAIS MAGUFULI ATEUA CAG MPYA ATAKAYECHUKUA NAFASI YA PROF ASSAD

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa katibu tawala mkoa wa Njombe Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Uteuzi huo unaanza kesho, Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa Assad ambaye imeelezwa kuwa muda wake wa uwongozi wa miaka mitano unaisha kesho Novemba 4, 2019.

Mteule huyo ambaye alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli ambaye alimteua tena na kumpeleka cheo cha chini kabisa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.

Akisoma taarifa ya uteuzi huo leo Jumapili Novemba 3, 2019, Balozi John Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama. Pia, Rais Magufuli amewateua Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu na majaji 12 wa Mahakama Kuu

Rais Magufuli alitengua uteuzi Charles Kichere Siku moja baada ya kukutana na wafanyabiashara, Ikulu Jijini Dar es Salaam ili kujadiliana changamoto mbalimbali za uendeshaji biashara nchini.