Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:48 am

NEWS: RAIS MAGUFULI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

DAR ES SALAAM: Rais John Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri lililoongezeka kutoka wizara 19 hadi 2I.

Wizara hizo zimeongezeka kutokana na wizara mbili kugawanywa huku nafasi za manaibu wapya zikiwa tano.



Akitangaza leo Jumamosi baraza hili jipya, Rais Magufuli amesema Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa mara mbili, sasa kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

Amesema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa rasilimali hiyo kwa taifa na kwamba wizara hizo zote kila moja itakuwa na waziri na naibu wake.

Rais Magufuli ametaja mabadiliko mengine katika Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo kwa sasa kutakuwa na Wizara ya Kilimo inayojitegemea na nyingine itakuwa ni Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Amesema sababu za kufanya mabadiliko hayo ni kutokana na umuhimu wa sekta hiyo inayoajiri asilimia 75 ya Watanzania nchini hivyo ni vyema ijitegemee. Kila wizara itakuwa na waziri na naibu wake.

Mabadiliko mengine ni katika wizara ya Tamisemi baada ya kuweka nafasi mbili za manaibu waziri kwa sababu ni wizara inayogusa sehemu kubwa ya wananchi.

Pia yamefanyika katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Angalia orodha ya mawaziri hao hapa

1.Wizara ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Waziri – George Huruma Mkuchik

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri – January Makamba

Naibu Waziri - Kangi Lugola

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri – Jenista Mhagama

Naibu Waziri – Anthony Peter Mavunde

Naibu Waziri Walemavu – Stela Alex Likupa

4.Wizara ya Kilimo

Waziri - Charles John Tizeba

Naibu Waziri - Mary Mwanjelwa

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri - Makame Mbarawa

Naibu Waziri - Atashasta Nditiye

Naibu Wziri - Elias John Kwandikwa

6.Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri - Dr Philip Mpango

Naibu Waziri - Dr Ashatu Kijaji

7.Wizara ya Nishati

Waziri - Medrad Matogoro Kalemani

Naibu Waziri - Subira Hamisi Mgalu

8. Wizara ya Madini

Wairi - Angela Kairuki

Naibu Waziri - Haroon Nyongo

9. Wizara ya Katiba na Sheria

Waziri – Palamagamba Kabudi

10. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri - Agustino Mahiga

Naibu Waziri - Dkt Susan Kolimba

11 .Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri - Dr Hussein Mwinyi

12. Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri – Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri - Hamad Masauni

13. Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Waziri - William Lukuvi

Naibu Waziri - Angelina Mabula

14. Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri – Hamisi Kigwangala

Naibu Waziri - Ngailonga Josephat

15. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Waziri - Charles Mwijage

Naibu Waziri - Stella Manyanya

16. Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi

Waziri - Joyce Ndalichako

Naibu Waziri - William Ole Nasha

17 .Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri – Ummy Mwalimu

Naibu Waziri – Faustine Ndugulile

18. Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri - Dr . Harrison Mwakyembe

Naibu Waziri - Juliana Shonza

19. Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri - Isack Kamwelwe

Naibu Waziri - .Juma Hamidu Aweso

20. Mifugo na Uvuvi

Waziri - Luhaga Mpina

Naibu Waziri - Abdallah Ulega

21. Wizara ya TAMISEMI

Waziri – Selemani Jafo