- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AMUAPISHA KICHERE KUWA CAG MPYA
RAIS Dk. John Magufuli, amemuapisha Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Profesa Mussa Assad ambaye kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kuwa muda wake Umekoma wa miaka 5.
Kichere ambaye aliwahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kabla ya kupangiwa majukumu mengine Juni 8, mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na Edwin Mhede.
Novemba 20,2016, Rais Dk. Magufuli alimteua Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA na Machi 25,2017 akateuliwa kuwa Kamishna Mkuu akichukua nafasi ya Alphayo Kidata.
Kichere alikuwa mtu wa nne kung’olewa kwenye kiti hicho ndani ya miaka minne, akitanguliwa na Rished Bade, Kidata na Dk. Philip Mpango.
Kutokana na kutenguliwa kwa uteuzi wake, Rais Dk. Magufuli alimteua kwa nafasi nyingine na kumpeleka kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
Kichere ametumikia nafasi hiyo kwa takribani miezi mitano, hadi uteuzi wa jana ulipofanyika.
Akitangaza uteuzi huo jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, alisema Rais Dk. Magufuli, amefanya uteuzi wa kujaza nafasi ya Profesa Assad ambaye muda wake wa miaka mitano unamalizika leo, Novemba 4.
“Kichere anachukua nafasi hii kuanzia tarehe 4 mwezi wa 11, akichukua nafasi ya Profesa Assad ambaye muda wake wa miaka mitano unakwisha kesho (leo) tarehe 4 mwezi wa 11, 2019. Kabla ya uteuzi huo Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe,” alisema Balozi Kijazi.
KAULI YA KICHEERE
Alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia uteuzi huo, Kicheere alisema “Namshukuru Mungu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na imani na kuniteua kwenye nafasi hii”
Kuhusu nini anawambia Watanzania alisema “Nitasema kesho (leo), baaa ya kuapishwa, niko njiani hatuwezi kuelewana kwa simu”
Waliowahi kuwa ma-CAG
Kichere anakuwa CAG wa saba nchini tangu Uhuru, baada ya R.W.A. McColl mwaka 1961 hadi 1963, Gordon Hutchinson mwaka 1964 hadi 1969, Mohamed Aboud mwaka 1969 hadi 1996, Thomas Kiama mwaka 1996 hadi 2005, Ludovick Utouh mwaka 2006 hadi 2014 na Profesa Mussa Juma Assad mwaka 2014 hadi 2019
Wasifu wa Kichere
Kichere ana Shahada ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es salaam Tanzania, Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) katika Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Diploma katika Usimamizi wa Fedha wa Miradi iliyofadhiliwa na wafadhili kutoka Kituo cha African Renaissance, Mbabane Swaziland, Shahada ya Biashara katika Uhasibu (B.Com Uhasibu) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye ni mwanachama wa Kamati za Mikopo na Ukaguzi.
Amekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe (RAS) hadi uteuzi mpya uliofanyika na Kamishna Mkuu wa zamani katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia amewahi kuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkuu wa Fedha na Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhakiki Mkuu wa Ndani wa Wakala wa Barabara za Tanzania (TANROADS), Mkaguzi wa Ndani wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkaguzi wa Ndani wa Kampuni ya Chai ya Unilever Tanzania Limited na Mkaguzi wa ndani / Mweka Hazina wa Kampuni ya Unilever Limited Kenya.