- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AMPA SIKU 7 RC MBEYA KUTETEA KIBARUA CHAKE
Mbeya: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amempa siku saba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila kuanzisha soko la dhahabu wilayani Chunya Mkoani Mbeya, huku akisema hili litakuwa jaribu lake kubwa kwa RC huyo kuendelea kuhudumu katika nafasi yake ya mkuu wa mkoa.
“Ninataka ndani ya siku saba hili soko liwe limeshafunguliwa hapa,’’ amesisitiza Rais Magufuli. Amesema kuwa haoni sababu ya mikoa mingine kushindwa kufungua masoko hayo wakati mkoa wa Geita walishafungua. “Kama mkuu wa mkoa wa Geita amefungua, sioni sababu kwa nini wakuu wa mikoa wengine ambako madini mbalimbali yanazalishwa wamekaa kimya, wanasubiri nini? Amehoji Rais Magufuli na kuongeza:
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Leo April 27, 2019 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Sabasaba wilayani Chunya mkoani Mbeya ambao ulikuwa unarushwa moja kwa moja (Live) na vyombo mbalimbali vya habari.
Amesema kuwa alishatoa maagizo kuwa kila mkoa ambao kuna uchimbaji wa madini ufungue kituo cha kuuzia dhahabu hivyo inashangaza kuona bado mikoa yote haijaanzisha isipokua mkoa wa Geita.
“Nilipokutana na viongozi wa madini pamoja na viongozi wa mikoa yote ya Tanzania Bara nilitoa maelekezo kwamba wakafungue masoko ya madini, tangu nimefika hapa (Chunya) sijaliona soko hilo,” amesema.
“Sasa nakuagiza mkuu wa mkoa (Albert Chalamila) pamoja na wizara hii (Wizara ya Madini), nataka soko la dhahabu hapa Chunya lianze, hakuna sababu ya soko hilo kutoanzishwa hapa Chunya,’’ amesema.
“Nimeshatoa maelekezo ni kutimiza, sasa mkuu wa mkoa jana nimeshakusifia lakini kwenye soko, hili litakuwa jaribu lako kubwa sana kwa shetani, mheshimiwa mkuu wa mkoa nakueleza hili sifurahi,” amemuambia RC Chalamila.
Pia, amewataka wakuu wa mikoa wengine ambao kwenye maeneo yao kuna uzalisjhaji wa madini wafungue vituo hivyo. ‘’Najua kuna wakuu wa mikoa wengine wananisikiliza, hawataki kufanya kazi, kama mkuu mkoa wa Geita ameweza wakuu wa mikoa mingine mnasubiri nini? Amehoji
“Na hili agizo si kwa mkuu wa mkoa tu wa Mbeya, wa Katavi ajiandae, wa Rukwa, Singida, Arusha ajiandae hivyo hivyo, siwezi kuwa na wakuu wa mikoa ambao natoa maagizo hawatekelezi, kwangu hapana,” amesisitiza Rais Magufuli kwa wakuu wa mikoa ambao maeneo yao yanachimbwa madini.