- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AMFUTA KAZI WAZIRI JANUARY MAKAMBA
Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano nchini Tanzania January Makamba na Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ambaye aliachia madarakani mara baada ya kashifa ya kuhusishwa na ripoti ya Madini ya Tanzanite.
Hata hivyo Taarifa ya Ikulu ya Tanzania haijaeleza sababu ya utenguzi wa Makamba.
Simbachawene anarejea kwenye baraza la mawaziri baada ya kujiuzulu uwaziri wa Nishati na Madini Septemba 2017 baada ya jina lake kutajwa kwenye kashfa ya kingia mkitaba ya madini iliyoitia hasara Tanzania.
Makamba ambaye ni kiongozi kijana atakumbukwa kwa kutumia madaraka yake kuweka suala la mifuko mbadala na kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki liyokuwa ikitajwa kwa kuongeza uchafua wa mazingira, hatua ambayo alifanikiwa kwa asilimia karibu 99%.
Simbachawene alijiuzulu baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya madini ya Tanzanite kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Bunge iliyoundwa kuchunguza biashara ya madini ya tanzanite, Dotto Biteko, alisema Simbachawene aulizwe ni kwa nini alitoa uhamisho wa hisa za Sky Associate bila kuhusisha wataalamu kwa sababu kamati ilishindwa kuelewa ni kwa nini alifanya hivyo.
“Kwa muktadha huo, ridhaa iliyotolewa Januari 30, mwaka 2015 na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, George Simbachawene, ina dosari za kisheria na ukiukwaji wa kiutendaji na utoaji wa ridhaa hii, unainyima Stamico kipaumbele cha kununua Kampuni ya TML.
Rais Magufuli pia amemteua Hussein Bashe, mbunge wa Nzega Mjini kushika nafasi ya Naibu Waziri wa Kilimo.
"Ndg zangu awali nimshukuru Allah kwa yote,namshukuru kwa dhati Mh Rais kwa imani yake, nijikumu zito nimelipokea kwa uwezo wa Allah tutavuka ni sector iloajiri Watanzania wengi na changamoto nyingi. Nawashukuru Watanzania wananchi wa Nzega na kwa dhati chama changu" amesema Hussein Bashe baada ya Kuteuliwa katika nafsi hiyo.
Kupitia mtandao wa Twitter, Makamba ameandika: "Ni kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo." Huku akiambatanisha maneno hayo na picha yake na rais msaafu Ally Hassan Mwinyi wakiwa wanaangua kicheko.
"Ndugu zangu Hussein Bashe na Simbachawene hongereni sana. Mungu awe nanyi katika majukumu haya mapya. Mazingira, Kilimo na Viwanda ndio nguzo muhimu za kujenga uchumi endelevu na fungamanishi. Nawapongeza sana." Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa.