Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:28 pm

NEWS: RAIS MAGUFULI AHAIDIWA MA BILIONI NA SEREKALI YA MAREKANI

Dar es salaam: Rais John Pombe Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson ambaye amesema Marekani itatoa fedha za nyongeza kiasi cha Dola Milioni 225 sawa na Shilingi Bilioni 499.500 za Tanzania katika mwaka ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo itakayogusa sekta za elimu, afya, lishe bora, utawala bora.

Mhe. Inmi Patterson amesema Marekani imeongeza fedha hizo katika miradi inayotekelezwa hapa nchini kwa sababu ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na Tanzania na itahakikisha uhusiano na ushirikiano huu unaendelezwa na kukuzwa zaidi.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Balozi Inmi Patterson kwa mchango mkubwa ambao Marekani imekuwa ikiutoa kwa Tanzania na amemhakiki kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano wake na Marekani, na pia amemuomba awahimize wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi wa Marekani waje kuwekeza na kufanya biashara hapa nchini kutokana na fursa lukuki zilizopo.

Mhe. Rais Magufuli pia ameiomba Marekani kusaidia kujenga hospitali kubwa ya kitaifa katika makao makuu ya nchi Mkoani Dodoma ili kuongeza uwezo wa Mkoa huo kutoa huduma za matibabu ikilinganishwa na ilivyo hizi sasa.