- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AGOMA KUMTIMUA KAZI DED SONGWE
Tunduma. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema amegoma kumfukuza kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilejem mkoani Songwe, Haji Mnas kwa kuwa hana taarifa za wizi zinazomhusisha mkurugenzi huyo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Oktoba 05, 2019 wakati akihutubia wananchi kwenye mji mdogo wa Mpemba ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Songwe.
Ametoa msimamo huo baada ya Mbunge wa Ileje (CCM), Janeth Mbene kusema mkurugenzi huyo hana ushirikiano na viongozi mbalimbali na kusababisha changamoto katika utendaji.
Mbene aliyewahi kuwa naibu waziri wa viwanda na biashara alipopewa amesema mkurugenzi huyo amekuwa hatoi ushirikiano kwa wenzake na hatekelezi majukumu yake ipasavyo na kwamba tatizo hilo limekuwa likielezwa kwa viongozi mbalimbali na pia mkoa umelifanyia kazi.
Akijibu tuhuma hizo, Rais Magufuli amesema ‘Kuhusu hili la mkurugenzi unajua kwa watu ambao hawaijui Ileje unaweza ukashangaa, sina uhakika kama dhambi zote hizo ni za mkurugenzi,” amesema na kuongeza
“Taarifa niliyonayo mimi, na (Seleman) Jafo (Waziri wa Tamisemi) ni shahidi kwamba huyu mkurugenzi saa nyingine anaacha kazi zake za ofisini anaenda kufundisha darasani.”
“Sasa mkurugenzi simtoi hadi nipate taarifa zangu mwenyewe, mkurugenzi uko hapa, sikutoi mpaka nipate information zangu mwenyewe,” amesema Magufuli huku mkurugenzi huyo akiwa amesimama kushukuru kwa kuinama
Rais Magufuli alimhoji Waziri Jafo kama ana taarifa za wizi zinazomkabili mkurugenzi huyo. “Una taarifa zozote za ubaya wa wizi, hela?” amemhoji
Akijibu swali hilo la Rais, Waziri Jafo amesema “Mh Rais katibu mkuu wetu ameunda timu ya kwenda kufanya uchunguzi wa ndani.”
Baada ya jibu la Jafo, Rais Magufuli amesema, “mnaona kumbe hata hiyo taarifa haijafika kwa Waziri wa Tamisemi, sasa mimi nichukue hatua tu yakufukuza mtu, ati jamani si nitawaonea watu kila mahali?.”