- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MAGUFULI AAGIZA KUKAMATWA MARA MOJA MKANDARASI RUKWA
Rais John Pombe Magufuli, ameagiza kukamatwa kwa mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa miradi ya maji mkoani Rukwa na akataka uchunguzi kufanyika mara moja ili kubaini waliokuwa wakimpa miradi hiyo.
Agizo hilo amelitoa Jana katika ziara yake mkoani Rukwa kabla ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga, Rais Magufuli aliagiza kukamatwa kwa mkandarasi huyo kwa kushindwa kutekeleza miradi ya maji yenye thamani ya Sh bilioni 1.7.
Alisema mradi huo uliotolewa kwa mkandarasi huyo kutoka kwa fedha za walipa kodi masikini wa Tanzania hadi sasa wananchi hawajapata maji, wakati mkataba wa Serikali na mkandarasi huyo akimaliza wananchi wapate maji na yeye apate fedha.
Alisema anashangazwa kuona mkandarasi huyo kupitia Kampuni ya Faric Contractors akiendelea kuwepo uraiani huku kukiwa hakuna juhudi zozote za kumchukulia hatua za kisheria.
“Hadi sasa maji hayapo na ninasikia mradi ukachomwa kabla hata haujakamilika, sola zaidi ya 150 zikaungua, vyombo vya dola vipo, PCCB ipo, Polisi wapo wala sijasikia wamepelekwa mahakamani, au wameshapelekwa mahakamani yeyote aliyechoma? Au kuna upelelezi bado unaendelea?” alihoji.
Mkuu huyo wa nchi, alitaka wahusika wote wakiwemo wa ubadhirifu wa mradi huo ambao wako nje kwa dhamana wakamatwe na warudishwe rumande na upelezi ukamilike ndani ya siku saba, kisha watuhumiwa wafikishwe mahakamani.
Aliwataka viongozi wa Polisi na PCCB kufanya uchunguzi haraka na kutoa muda wa siku saba
“Inachukua muda gani kuwapeleka mahakamani? Waghusika waliokamatwa wako wapi? kwa nini wakae nje kwa dhamana wakati hizi fedha bilioni 1.7 zimepotea wananchi hawa wanakosa maji, inawezekana wengine wamekunywa maji yenye magonjwa wanakufa, huyu yuko nje kwa dhamana tu anatembea, tuma askari wako sasa hivi wamkamkamate wamweke ndani.
“Nawapa siku saba, wewe wa PCCB RPC na wengine wote wanaohusika muhakikishe haya munayamaliza, kama ni kupelekwa mahakamani wapelekwe, miezi miwili mnapeleleza tu? Msinifanye nichukue hatua za ajali, na nitafuatilia mwenyewe,” alisema
Alimtaka Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, kuwafuatilia watu wote wanaohusika kumpa miradi hiyo mkandarasi huyo ambaye amekuwa akipata miradi hiyo na kwamba watu wa manunuzi na Bodi ya Wakandarasi wahakikishe miradi yote inatathminiwa upya.
“Na katika hili nitaondoka na mtu, nawahakikishia,” alisistiza