- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS KIM AJITOKEZA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya siku 20 za kutoonekana hadharani.
Shirika la Habari la Korea Kaskazini KCNA limemuonesha leo Kiongozi huyo akikata utepe wakati akifungua kiwanda cha Mbolea.
KCNA limesema wafanyakazi katika kiwanda cha mbolea walianza ," kushangilia kwa nguvu na furaha baada ya kumuona kiongozi wao".Rais Kim akifurahi jambo baada ya kukata utepe.
shirika hilo lilisema , analiongoza taifa hilo katika mapambano ya ujenzi wa uchumi wa kujitegemea kutokana na "upepo mkali unaokuja" kutoka kwa "nguvu hasimu."
Ripoti hiyo haikueleza maelezo ya moja kwa moja kuelekea Washington ama Seoul
JE Trump anasemaje baada ya kim kuonekana.
Akizungumza na waandishi habari leo katika Ikulu ya White House, rais wa Marekani Donald Trump hakutaka kueleza chochote kuhusu kujitokeza kwa Kim lakini alisema , atakuwa na kitu cha kusema juu ya hilo katika wakati muafaka.
Vyombo vya habari vya taifa viliripoti kwamba Kim anafanya shughuli za kawaida bila kutoka hadharani, kama kutuma salama kwa viongozi wa Syria, Cuba na Afrika kusini na kuelezea shukurani zake kwa wafanyakazi wanaojenga maeneo ya kitalii katika mji wa pwani wa Wonsan, ambako baadhi ya watu walisema anaishi huko.
Serikali ya Korea kusini , ambayo ina rekodi mchanganyiko za kuwafuatilia viongozi wa ngazi ya juu wa Korea kaskazini , imekuwa mara kwa mara ikipuuzia minong'ono kuwa Kim, anayeaminika kuwa na umri wa miaka 36, alikuwa katika hali mbaya ya kiafya kutokana na upasuaji aliofanyiwa.
Imeandikwa na Joyce Liliam
Muakilishi Publisher