- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS KENYATTA AFANYA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri. Katika hotuba yake ya kwanza katika mwaka wa 2020 aliyoitoa kwenye Ikulu ya Rais Mombasa.
Katika mabadiliko hayo, yaliyofanyika jana wanawake wameonekana kuchukua nafasi muhimu ambapo Monica Juma ambaye awalikuwa waziri wa mambo ya nje amechukua wadhifa wa waziri wa ulinzi huku Raychelle Omamo aliyekuwa waziri wa ulinzi akiwa waziri wa mambo ya nje.
Ukur Yatani amedumisha wadhifa wake wa waziri wa fedha, Mutahi Kagwe ambaye aliwahi kuhudumu katika serikali ya Kenyatta amerejeshwa tena kama waziri wa Afya.
Betty Maina ambaye ametoka sekta ya biashara ameteuliwa kuwa waziri wa viwanda na Sicily Kariuki aliyekuwa waziri wa afya akiwa waziri wa maji.
Esther Koimett waziri wa habari na mawasiliano naye Simon Chelugui ni waziri wa Leba.
Peter Munya ndio Waziri wa kilimo huku Mwangi Kiunjuri akipigwa kalamu na wengineo.
Wakati wa hotuba yake Rais amesema kwamba wanaweka mipango ya kukwamua uchumi na kuweka wazi kuwa asilimia 70 ya madeni yamelipwa.