- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS KAGAME ASHINDA KWA KISHINDA
Kigali: Raisi wa Rwanda Paul Kagame ameshinda kwa asilimia 98 ya kura kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi jumamosi. uchaguzi huo uliofanyika Jana siku ya ijumaa tarehe 4 Agosti 2017.
Katika asilimia 80 ya kura zilizohesabiwa raisi Kagame amepata kiasi cha kura milioni 5.4 akivuka asilimia 51 zilizotakiwa ili mshindi kupatikana.
Tume ya uchaguzi imekadiria kufikia asilimia 97 ya kura milioni sita nukta tisa ya watu wote waliopiga kura.
Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Rwanda Kalisa Mbanda amesema hatarajii matokeo hayo kubadilika hata baada ya kuhesabu asilimia zote za kura.
Aidha mgombea Frank Habineza wa chama pekee kilichoruhusiwa kufanya upinzani nchini humo cha Democratic Green amejipatia asilimia 0.45 ya kura huku mgombea binafsi Philippe Mpayimana akipata 0.72.