- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS HOSNI MUBARAK KUZIKWA LEO KIJESHI MJINI CAIRO
Misri inafanya mazishi ya heshima za kijeshi, ya aliyekuwa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani wakati wa wimbi la vuguvugu la maandamano ya umma katika ulimwengu wa Kiarabu. Mubarak, ambaye aliitawala Misri kwa miongo mitatu, alifariki dunia jana katika hospitali moja ya mjini Cairo akiwa na umri wa miaka 91.
Televisheni ya taifa imesema maafisa wa ngazi ya juu wamealikwa kuhudhuria mazishi hayo ya kijeshi, bila kutoa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa ripoti za vyomvo vya habari, Mubarak atazikwa katika eneo la makaburi ya familia mjini Cairo.
Kiongozi huyo wa zamani na wanawe wawili walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani na kutakiwa kulipa faini ya mamilioni ya dola kwa ubadhirifu wa pesa za serikali. Mubarak alitumikia muda mwingi wa kifungo chake hicho hospitalini, na hatimaye kuachiliwa huru mnamo mwkaa 2017.