- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS ERDOGAN AELEKEA KUPOTEZA MAMLAKA NCHINI UTURUKI
Chama cha AKP cha rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kimeanguka vibaya mjini Ankara na kinaelekea kuupoteza pia mji wa kibiashara wa Istanbul kwenye Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaoendelea nchini humo.
Mchakato wa kuhesabu kura katika uchaguzi muhimu wa serikali ya mitaa nchini Uturuki unaendelea lakini tayari zimeshajitokeza dalili kwamba kwa mara ya kwanza rais Recep Tayyip Erdogan na chama chake kinachotawala wanakabiliwa na hali ngumu ya kuelekea kushindwa.
Mkuu wa tume ya uchaguzi tayari ameshasema leo asubuhi kwamba upinzani unaoongoza katika matokeo ya uchaguzi katika mji wa Istanbul wakati ambapo kura bado zinaendelea kuhesabiwa katika mji huo wa historia ya utamaduni na kibiashara nchini Uturuki,mji ambao umekuwa kwa miaka yote tangu 1994 alipochaguliwa Erdogana kuwa meya wa jiji hilo ukishikiliwa na kambi ya waislamu wahafidhina.
Kwa mujibu wa matokeo yasiyokuwa rasmi chama cha haki na maendeleo AKP kimepoteza udhibiti katika mji mkuu Ankara abao pia toka mwaka 1994 ulikuwa mikononi mwa chama hicho tawala. Mkuu wa tume ya uchaguzi Sadi Guven anasema hadi sasa katika mji wa kibiashara wa Istanbul kura za masanduku chungunzima zimeshahebabiwa na kura zilizobakia ni za masanduku manane tu,kutokana na malalamiko yaliyoibuka juu ya masanduku hayo.