- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS BUHARI ASHINDA TENA KITI CHA URAIS NCHINI NIGERIA
Tume ya uchaguzi nchini Nigeria (INEC) imemtangaza Rais anayemaliza muda wake nchini Nigeria Muhammadu Buhari kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi Februari 23. Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Buhari amepata 56% ya kura zote dhidi ya Mahasimu wake wa Upinzani waliopata kura 41%.
Muhammadu Buhari amechaguliwa tena kuingoza nchi hiyo kwa mihula minne ijayo.
Hata hivyo awali upinzani ulilalama kwamba kuna njama ya kuiba kura na kubaini kwamba hautokubali matokeo ya uchaguzi
Muhammadu Buhari ameshinda kwa kishindo katika majimbo ya Kaskazini, ambapo wakazi wao majimbo hao ni wengi. katika Jimbo la Kano, amepata kura milioni 1.4, sawa na katika Jimbo la Katsina ambako anazaliwa.
Pia amepata ushindi mkubwa katika Majimbo ya Bauchi, Borno, Yobe, Zamfara na Kaduna.
Buhari mwenye umri wa miaka 76 amemshida mpinzani wake mkuu na aliyekua makamu wa rais bwana Atiku Aboubakar.
Chama cha Buhari kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.
Asilimia 35 tuu ya wapiga kura walijitokeza , baadhi wafuasi wa Buhari tayari wameingia mtaani kushangilia.
Buhari alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 akiwa ni kiongozi wa kwanza wa upinzani kukalia kiti cha urais.